MWANA MAMA VICKY
NTETEMA.
Katika safu yetu ya Mwana Mama, leo tunawaletea
Vicky Ntetema, mwandishi wa habari wa kimataifa na mtetezi wa haki za Binadamu.
Jina la mama huyu lilivuma sana wakati akitangaza shirika la habari la BBC, kwa
wengi alijulikana kama mama mwenye sauti nzuri ya kumtoa nyoka pangoni. Kila
mtu mpenda habari alitamani kukutana na mama
huyu ambaye daima alitumia kiswahili fasaha na sauti yenye kumvuta mtu
kuendelea kumsikiliza.
Mwana mama huyu ni miongoni mwa waandishi wa habari
wachache wa Afrika, ambao wamefanikiwa kufanya mahojiano na vingozi mbali mbali
wa nchi na watu wengine wengi maarufu
Afrika na duniani kote. Ni mwandishi ambaye hakusita kumbana mtu
anayehojiana naye hadi kufanikisha lengo lake au jibu alilolikusudia. Inawezekana
aliwaudhi baadhi ya watu waliohojiano nao, lakini hapana shaka kwamba daima
aliwafurahisha wasikilizaji wake.
Mbali na mama huyu kusikika akitanga Sauti ya idhaa ya Kiswahili BBC, jina lake
limetokea kuwa maarufu sana alipojitokeza kutangaza na kufichua unyama
waliokuwa wakitendewa walemavu wangozi, maalibino. Utafiti alioufanya juu ya
suala hili la mauaji ya Albino, ulifichua uwezo wake wa kufanya uchunguzi,
ushupavu wa kuusimamia ukweli, kuuelezea na kuutetea. Mauaji ya Albino ni mradi
ulioendeshwa na wauaji, ambao walikuwa tayari kutoa roho ya mtu yeyote Yule
ambaye angejiingiza kwenye anga zao. Hawa ni matajiri wenye hela ambao wanaweza
kumshukughulikia mtu wakati wowote. Vicky Ntetema, hakuogopa vitisho hivyo,
aliendelea na uchunguzi wake hadi kufikia hatua ya kutengeneza vipindi na
kuvirusha hewani.
Binafsi, nilipat bahati ya kukutana na mama huyu
akiwa anafanya utafiti wake kule Magu Mwanza. Unyenyekevu wake, ulinisukuma
kuzoeana naye kwa haraka, na sisi mimi tu niliyezoeana naye, bali watu wengi
aliokutana nao, na labda ndo maana aliweza kufanikisha utafikti wake ambao
ulikuwa umezungukwa na vitisho vya kila aina.
0 comments:
Post a Comment