MAUAJI YA KIMBALI YA RWANDA, NANI WA KUJIFUNZA?

Naandika makala hii kulaani mauaji ya kimbali yaliyotokea Rwanda 1994. Yalikuwa ni mauaji ya kinyama yaliyolenga kuwafuta Watutsi katika uso wa dunia ni “Lazima” yalaaniwe na kila mwanadamu mpenda amani. Ingawa mauaji haya yalipotokea nilikuwa ninaishi Karagwe, jirani kabisa na nchi ya Rwanda; nilishuhudia maiti waliokuwa wakielea kwenye mto Kagera, niliwapokea wakimbizi na kuishi nao, niliyasikiliza yote waliyokuwa wakisimulia wakimbizi hao, nimesoma maandishi mengi na kuangalia filamu juu ya mauaji ya Rwanda; nilikuwa sijapata picha kamili ya mauaji hayo mpaka juzi tarehe 17.10.2011 nilipotembelea makumbusho ya mauaji ya kimbali.

Makala mbili zilizotangulia, nilielezea safari ya Kigali na sherehe za Kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere. Nilielezea maendeleo ya kasi nchini Rwanda chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Rais Paul Kagame. Wanyarwanda wakikuonyesha maendeleo yao; nyumba za kisasa, usafi wa jiji lao la Kigali na miji mingine, huduma ya maji, shule, hospitali na kukuhakikishia kwamba sasa nchi ina amani na utulivu, watahitimisha ziara kwa kupeleka kwenye makumbusho ya mauaji ya kimbali. Hawawezi kusahau tukio hilo, imebaki kuwa kumbukumbu isiofutika. Wanasamehe yaliyotokea, lakini kamwe hawawezi kusahau. Hivyo nahitimisha makala zangu juu ya safari ya Rwanda, kwa kuandika juu ya Makumbusho ya mauaji ya kimbali. Swali langu kubwa likiwa: Mauaji ya Kimbali Rwanda, nani wa kujifunza.

Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Balozi Dkt. Matiko, alitwambia “ Mwezi wa nne, kila mwaka ni juma zima la kukumbuka ya mauaji ya kimbali. Kila kitu hapa kinakufa ganzi. Hakuna shughuli zinazoendelea. Taifa linakuwa kwenye majonzi makubwa ya kukumbuka ndugu zao waliopoteza maisha yao wakati wa mauaji ya kimbali”.

Rwanda ina vituo vingi vya Makumbusho ya mauaji ya kimbali, sisi tulitembelea vituo viwili, kituo cha Nyamata na Ntarama. Vituo hivi viko kwenye eneo la Bugesera, ambako kulikuwa na Watutsi wengi. Historia ni kwamba baada ya ile vita ya 1959, watawala wa Kihutu waliamua Watutsi wapelekwe Bugesera ili wafe kwa kushambuliwa na mbungo. Walikufa wachache wakati ule, maana walipata mbinu za kupambana na mbungo mpaka mauaji ya kimbali yalipowakuta.

Nyamata, ilikuwa ni parokia ya Kanisa katoliki na Ntarama kilikuwa ni kigango cha parokia ya Nyamata. Ndani ya kanisa la Nyamata, waliuawa watu elfu kumi (10000) na miili ya watu hawa imetunzwa kwenye kanisa hili. Kigango cha Ntarama waliuawa watu elfu tano (5000) na miili ya watu hawa na vitu vyao kama vile nguo, viatu, magodoro, vifaa vya maji bado vinatunzwa kwenye kanisa hili dogo.

Vifaa vilivyotumika kwa mauaji, kama mapanga, nyundo na vijiti walivyokuwa wakiwaingizia wanawake sehemu za siri hadi vinatokea mdomoni, bado vimetunzwa. Damu zilizotapakaa kwenye makanisa hayo bado zinaonekana na hasa sehemu ambapo watoto wadogo walikuwa wakibamizwa hadi vichwa vinapasuka, damu iliyokauka inaonekana kwenye ukuta na kuashiria kwamba watoto wengi walikufa kwa kubamizwa kwenye ukuta.

Makanisa haya mawili hayatumiki tena kwa ibada. Yamebaki kama vituo vya makumbusho ya mauaji ya kimbali. Wamejitahidi kuacha kila kitu kilivyokuwa mwaka 1994, ingawa kwenye kanisa la Nyamata, wamejenga kaburi kubwa chini ya kanisa, kutunzia mabaki ya miili ya wahanga wa mauaji ya kimbali. Pia nje ya kanisa la Nyamata, wamejenga kaburi kubwa ambalo mtu unaweza kuingia na kushuhudia mwenyewe mabaki ya miili ya wahanga wa mauaji ya kimbali.

Mwili wa Mwanamke, aliyebakwa na wanaume 20, na baadaye kuteswa ahadi kufa kwa kuwekewa kijiti sehemu za siri na kutokea mdomoni umetunzwa kwenye kanisa la Nyamata. Mauaji na mateso ya kutisha yalitokea kanisani na kuna ushahidi kwamba watu wengi waliuawa juu ya Altare, meza ambayo kila Jumapili padri wao alikuwa akisimama na kugeuza mkate kuwa mwili wa Bwana, na divai kuwa damu ya Yesu; watu wote wa Nyamata, waliouawa na walioua walikuwa kila Jumapili wakikutana kwenye kanisa hilo kusali pamoja.

Watu walikimbilia kanisa kupata ulinzi. Miaka ya nyuma makanisa ndo yalikuwa kimbilio. Waliamini hakuna baya linaweza kutokea kanisani. Wauaji walitumia mbinu hiyo kuwahadaa Watutsi kukimbilia kanisani, ili wapate njia nzuri ya kutekeleza mauaji yao. Baada ya kuhakikisha idadi kubwa imeingia kanisani, walitoa taarifa kwa jeshi. Hivyo kwa kiasi kikubwa mauaji ya Nyamata na Ntarama, yalifanywa na Jeshi. Mabaki ya risasi na mabomu kwenye kanisa la Nyamata, matundu ya risasi kwenye kuta, milango na paa la kanisa hilo ni ushahidi wa kutosha kwamba mauaji hayo hayakutekelezwa kwa mapanga na nyundo tu bali hata kwa risasi na mabomu.

Risasi hazikuangalia Mwili ya Kristu, maana kwenye kanisa hilo la Nyamata, kisanduku(Tabenakulo) kinachotumika kuhifadhi mwili wa Kristu, kilicharazwa risasi, na ni wazi hostia (Mwili wa Kristu) zilimwagika chini. Bwana Yesu, akawaacha watu wake kuchinjana mbele yake! Sanamu ya Bikira Maria, mama wa shauri jema, mama wa huruma na upendo, kwenye kanisa hilo nayo ilicharazwa risasi! Sanamu hiyo bado ipo hapo kanisani na “majeraha” yake! Hapana shaka kwamba ukatili wa kutisha ulifanywa kwenye kanisa hilo.

Binti anayewapokea wageni na kuwaelezea yaliyotokea hapo Nyamata, alikuwa na umri wa miaka 8 mauaji yalipotokea. Ana kumbukumbu ya mauaji hayo yaliyotekelezwa ndani ya siku mbili tu. Baada ya kututembeza, kutuonyesha masalia ya miili na kutuelezea kwa kirefu yaliyotokea Nyamata, alituuliza swali gumu ambalo hatukupata jibu lake: “ Baada ya kutembelea makumbusho haya, mna ushauri gani? Je ni vizuri kuendelea kuonyesha masalia ya miili ya wahanga wa Mauaji ya kimbali, au tuizike na kufunika kabisa na kuisahau historia hii ya uchungu? Mnatushauri nini ndugu zetu kutoka Tanzania?”

Hakuna jibu lililotoka. Tulitizamana sote na kasha kimya kilitawala. Ni wazi kila mtu alikuwa na jibu lake. Tulipokuwa kwenye gari tukirudi hotelini tulikofikia, mjadala ulianza: wengine walisema “ Ni bora kuifunika miili na kuacha kuonyesha, maana kuionyesha kunaweza kuchochea hasira” wengine na hasa wakereketwa wa “amani” walisema “ isifunikwe ili watu waone na kujifunza kutochezea amani”. Ni imani yangu hata wewe msomaji wa makala hii utakuwa na maoni yako kuhusu jambo hili. Unaweza kutoa maoni yako, Wanyarwanda ni wasikifu, watasikia.

Tulikuwa kama watanzania ishirini na tano tuliotembelea makumbusho haya ya Nyamata na Ntarama. Kila mtu alikuwa na la kwake moyoni. Kilichokuwa wazi ni kwamba simanzi, hofu na huzuni vilimgusa kila mmoja wetu. Kila mmoja wetu alionyesha kuchukizwa na unyama uliotendeka kanisani. Mimi binafsi nilikuwa na maswali mengi kichwani mwangu: Kwa nini mauaji haya yalitokea kanisani? Je, leo hii Kanisa Katoliki la Rwanda lina mbinu gani za kutibu majeraha haya na kama kanisa lina msimamo gani juu ya makumbusho ya mauaji ya kimbali ambayo yako kwenye makanisa yao? Wana nguvu za kuweza kusimama na kuhubiri? Je kwa nini roho ya mtu igeuke na kuwa kama ya mnyama? Haingii akilini kwamba vitendo vya Nyamata na Ntarama vilitendwa na binadamu. Kwa nini watu walifikia hatua hiyo? Ni propaganda za kisiasa? Ni siasa mbaya? Ni uongozi na utawala mbovu ni nini?

Tulielezwa kwamba kwenye makanisa mengine yalikotokea mauaji, hata mapadri walishiriki mauaji. Waliwatenga Wanyarwanda kwenye makundi ya Wahutu na Watutsi, na kuwaruhusu wanajeshi kuwaua Watutsi. Baadhi ya mapadri hawa bado wanaishi na kuhubiri neno la Mungu Rwanda. Na la kushangaza ni kwamba makanisa yanajaa waumini, nilipouliza, niliambiwa “ Wanyarwanda wanapenda sana dini”

Wakati mimi nikitafakari ya kwangu na wenzangu walikuwa wakitafakari pia. Huwezi kutembelea Nyamata au vituo vingine vya mauaji ya kimbali ukatoka bila tafakuri nzito. Wenzetu wengine ilibidi wameze vidonge vya kuteremsha shinikizo la damu na wengine niliona wakimeza panadol kutuliza maumivu ya kichwa baada ya kushuhudia unyama unaoweza kutendwa na binadamu. Baadhi ya wenzetu walisikika wakisema kwa masikitiko “ Watanzania wenzetu wasiopenda amani, waje hapa Nyamata na Ntarama wajifunze”.

Swali langu kwao likawa “ Ni watanzania gani wasiopenda amani”. Jibu likawa “ Wale wanaopenda maandamano”.

Nafikiri tusijidanganye. Mauaji ya kimbali ya Rwanda, ni fundisho letu sote. Ni fundisho kwa chama tawala cha CCM na ni fundisho kwa wapinzani pia. Ni lazima kutambua kwamba binadamu ni binadamu, awe CCM au upinzani anabaki kuwa yule yule; mwenye tamaa, mwenye wivu, mwenye kiburi, mwenye ubaguzi, mwenye mashindano, mwenye kutaka madaraka, mwenye kutaka kuwanyanyasa wengine, mwenye kutaka kuwa bora zaidi ya wengine. Hivyo mwanadamu ni lazima aongozwe na vitu kama sheria, katiba, kanuni, utamaduni, mila na desturi. Na haya ni lazima kuyajenga pamoja kama taifa na kila mtu lazima awe na mchango wake na ni lazima kila mtu kuyafuata na kuyaheshimu. Nchi si mali ya mtu au kikundi chochote cha kisiasa. Ni imani yangu kwamba hakuna mtu asiyependa Amani. Sote tunapenda amani, ndo maana ninasema ni jambo muhimu sote kujifunza matokeo ya uvunjifu wa amani kutoka Rwanda.

Matukio ya Igunga, ya wanasiasa kupanda jukwaani na bastola, si kupenda amani! Kununua shahada za watu ili  wasipige kura si kupenda amani, maana watu hawa wakitaka kupiga kura kwa nguvu, amani itapotea. Serikali kuingiza nchi kwenye mikataba mibovu, si kupenda amani, maana kuna siku wananchi watasimama na kuikataa mikataba hii, na hili likitokea hakuna amani. Kupora ardhi kwa visingizio vya uwekezaji si kupenda amani, maana wananchi wakisimama kudai ardhi yao amani itapotea.

Tusipokuwa na chakula cha kutosha, amani itapotea! Mtu mwenye njaa hawezi kuwa na amani. Bidhaa muhimu zinapanda bei usiku na mchana; mafuta ya taa yanapanda bei, sukari inapanda bei na vyakula sasa vinapanda bei. Hatuwezi kuwa na amani , kama wananchi watakuwa hawana bidhaa muhimu katika maisha yao ya kila siku. Amani itavunjika pole pole na hatimaye inaweza kufikia kilele kama kile cha Nyamata.

Tusiwatupie lawama  wale wanaopenda maandamano. Tujiangalie kama taifa tunaelekea wapi? Tunajenga taifa la kuvunja amani siku za mbele au tunaweka misingi imara ya kulinda amani na utulivu? Tumeanza kujenga matabaka ya walionacho na wasiokuwa nacho, ufa unakuwa mkubwa kila kukicha. Tunajenga sekondari za kata na kuacha watoto wa vigogo kusoma shule nzuri na nje ya nchi. Je watoto hawa kesho na keshokutwa watapikika chungu kimoja? Hatuna mpango mzuri wa kuwaingiza kwenye jamii watoto wa mitaani. Tunawaacha wanakulia mitaani, wanaoa na kuolewa na kutengeneza familia wakiwa mitaani. Siku ya siku hawa watakuwa salama yetu?

Tusipoziba ufa tutajenga ukuta! Tusikwepe wajibu wetu, kujenga amani ni kazi yetu sote. Kama kuna la kujifunza juu ya kuilinda amani ni lazima tujifunze wote. Kwa maana hiyo mauaji ya kimbali ya Rwanda ni fundisho kwa watanzania wote.

Na,
Padri Privatus Karugendo.

+255 754 6331 22.

KIFO CHA MUAMMAR GADDAFI NI KIFO CHA UHURU WA AFRIKA

Jumapili iliyopita yalitokea makosa katika safu yangu ya Tusemezane. Makala iliyotokea hapo juu ya Muammar Gaddafi, haikuwa yangu. Nafikiri ni kazi ya mhariri kuwaelezea wasomaji kilichotokea. Nilipokea simu na sms nyingi. Wengine wakinipongeza, wengine wakinilaumu na kunitukana. Kilichonisikitisha, pamoja na makosa ya uhariri, ni kwamba makala iliyowekwa kwenye safu yangu ilikuwa na mawazo na msimamo tofauti na wa kwangu juu ya maisha ya Muammar Gaddafi. Maana yake wale waliokuwa wananipongeza kwa makala nzuri, ni kwamba mimi si sitahiri hizo pongezi na wale walionitukana walinionea bure! Sikuweza kuwajibu wote; hivyo nina imani makala ya leo ni jibu. Huu ndio msimamo wangu juu ya kuawa kwa Muammar Gaddafi.

Afrika tulitawaliwa na tuliuzwa sokoni kama bidhaa nyinginezo. Utumwa na ukoloni ni historia mbaya katika historia ya dunia yetu. Hadi leo hii wakoloni, walishindwa kuomba msamaha kwa dhambi kubwa walizotutendea. Inajulikana wazi kwamba walitupatia uhuru shingo upande na kuendelea kututawala kwa njia mpya za utandawazi, soko huria na ukoloni mambo leo kama ilivyojitokeza juzi kwa Waziri Mkuu wa Uingereza kutamka wazi kwamba bila kuukubali ushoga hatutapata misaada!

Viongozi wa Afrika walioonyesha kuwa na mwanga wa kutaka uhuru kamili walizimwa. Mfano mzuri ni wa Patrice Lumumba. Hata akina Nkrumah, kupinduliwa kwao kulikuwa na msukumo wa hawa mabwana wakubwa. Wana ujanja wa kutumia misemo kama Demokrasi, haki za binadamu, kulinda maisha ya watu na upuuzi mwingine mwingi, huku wakiuma na kupuliza. Lengo lao ni kuwapumbaza  Waafrika, kuendelea kuwatawala na kuwafanya soko lao kubwa na sehemu ya kuchuma rasilimali nyingi kama vile mbao, madini, ardhi ya kulima chakula na kuzalisha nishati, sehemu za kupumzikia na mengine mengi.

Kilele cha hujuma za wakoloni kimejionyesha wazi kwa kifo cha Muammar Gaddafi, aliyekuwa rais wa Libya. Shutuma zote juu yake kwamba alikuwa dikteta, kwamba alikuwa anawaua watu wake, kwamba alikuwa akisaidia makundi ya kigaidi ni uongo mtupu. Gaddafi, alikataa kuwauzia mafuta Wazungu kwa dola, yeye alitaka awauzie kwa dhahabu. Walete dhahabu awapatie mafuta. Gaddafi, alikataa makampuni ya kigeni kuja Libya kuchimba mafuta. Alisimama imara na kusema wao wana makampuni yao ya kuchimba mafuta. Wazungu, waje wanunue mafuta na si kuja kuchimba mafuta Libya. Gaddafi, alitaka Afrika kuungana. Alitaka Afrika iwe na serikali moja, ili bara letu liwe na nguvu na kuweza kushindana na hawa wakoloni. Alikuwa tayari kutoa fedha ili kutekeleza mradi huu mkubwa na wenye manufaa makubwa kwa bara zima la Afrika. Wakoloni hawakuyataka mawazo yake haya na sasa wamehakikisha ameondoka na kufutika! Ni unyama ule ule wa Ukoloni na utumwa.

Kifo cha Gaddafi, kimewasikitisha wengi na hasa Waafrika ambao wanatambua mchango wake mkubwa. Kama alivyosema Waziri Membe, ni kichaa peke yake anayeweza kusimama na kusema kwamba Gaddafi, hakufanya kitu. Sote tunakumbuka alivyoligeuza jangwa kuwa kijani, sote tunajua jinsi ambavyo watu wake wasiokuwa na kazi walivyokuwa wakipata posho ya kujikimu, tunajua jinsi alivyowajengea wananchi wake makazi bora ya kuishi, sote tunajua jinsi alivyoigeuza Libya kuwa ni nchi yenye maendeleo makubwa ndani ya bara la Afrika. Ametoa michango mingi kwenye nchi mbali mbali za Afrika. Amekuwa akitoa fedha za kuuendesha mikutano ya Umoja wa Afrika. Ni mtu aliyewapenda watu wake wa Libya na ni mtu aliyelipenda bara letu la Afrika. Kifo cha kinyama kilichomfika ni aibu na laana kubwa kwa watu wa Libya kukubali kutumiwa na wakoloni kutekeleza adhima yao.

Kama kweli wakoloni walikuwa na nia njema, mbona nguvu zilizotumika Libya kumuondoa Gaddafi, hazitumiki mashariki ya kati? Mbona Syria, kuna maandamano ya kuikataa serikali iliyo madarakani kuondoka na watu wengi wamekufa, lakini hatujaona nguvu kubwa zikitumika kama zile zilizotumika Libya?

Wanataka mafuta ya Libya! Wanataka rasilimali za Afrika, wanataka soko la Afrika; wanataka Afrika isiungane na kuwa na nguvu ili waendelee kutugawanya na kututawala. Wanataka kuendeleza ukoloni na utumwa, wanataka kuzirudia sera za mababu zao zilizoliteketeza bara la Afrika.

Wapo watanzania wenzetu wanasema Gaddafi, alikuwa mbaya maana alishirikiana na Iddi Amin kuivamia nchi yetu. Ni kweli alifanya vibaya, hata yeye alijuta na kuomba msamaha. Hizo zilikuwa ni siasa. Hata sisi Tanzania wakati wa vita ya Biafra, pamoja na msimamo wa Tanzania wa kutaka umoja, tulisimama upande wa Biafra wa kutaka Nigeria igawanywe vipande  viwili. Mwalimu Nyerere, alikuwa na hoja nzuri na alijielezea vizuri. Msimamo wetu huo juu ya Biafra, haukutufanya tuonekane maadui wa Nigeria. Hata hivyo kwani ni Gaddafi peke yake alimsaidia Iddi Amin wakati wa vita ya Kagera?

Hakuna anayesema kwamba Gaddafi, alikuwa mtakatifu. Alikuwa na mapungufu yake kama binadamu wengine wote. Lakini kwa suala la kujenga taifa huru lenye maamuzi yake, kwa suala wa umoja wa Afrika, kwa suala  la rasilimali za Afrika kuwanufaisha Waafrika wenyewe, hakuwa na mfano wake. Kama tuna bishi tusubiri utawala mpya wa Libya ndo tutatambua kazi kubwa iliyofanywa na Gaddafi.

Kwamba alikuwa akieneza Uislamu, hilo si kosa maana kila muumini ana wajibu wa kuieneza dini yake. Miaka mingi Waislamu na Wakristu wameeneza dini zao ndani ya bara la Afrika, lakini ukweli usiopingika ni kwamba hadi leo hii bado kuna Waafrika wanaoamini bado dini zao za jadi. Hawakukubali kuingia kwenye Uislamu ama Ukristu. Kueneza na kupokelewa ni vitu viwili tofauti; watu wakikubali kupokea imani fulani, maana yake ni kwamba wameilewa na kuipenda; kama si kuwalazimisha watu kwa upanga kama ilivyofanywa miaka ya nyuma katika Bara letu la Afrika  na Amerika ya kusini, hakuna tatizo la mtu kuipokea imani anayoamini itaboresha utu wake na kumwongoza kuishi vyema na binadamu wenzake.

Kifo cha Gaddafi, kitufumbue macho. Ni lazima Waafrika kushikamana na kusema hapana! Ni lazima kukataa mbinu hizi za wakoloni kutaka kutuchagulia viongozi. Ni lazima kuwakataa hawa vibaraka wao na kuwa tayari kulilinda bara letu la Afrika, ili liwe salama kwa vizazi vijavyo. Ni bora kufa tukilitetea bara letu kuliko kuliacha likachukuliwa na hawa wakoloni wajanja wanaojifanya wanaipenda sana Afrika kumbe ni mbinu za kuhakikisha bara letu linabaki gizani na kuendelea kunyonywa. Uhuru wetu unakufa ni lazima tusimame kidete kuutetea.

Na,
Padri Privatus Karugendo

MAUAJI YA KIMBALI YA RWANDA, NANI WA KUJIFUNZA?

Naandika makala hii kulaani mauaji ya kimbali yaliyotokea Rwanda 1994. Yalikuwa ni mauaji ya kinyama yaliyolenga kuwafuta Watutsi katika uso wa dunia ni “Lazima” yalaaniwe na kila mwanadamu mpenda amani. Ingawa mauaji haya yalipotokea nilikuwa ninaishi Karagwe, jirani kabisa na nchi ya Rwanda; nilishuhudia maiti waliokuwa wakielea kwenye mto Kagera, niliwapokea wakimbizi na kuishi nao, niliyasikiliza yote waliyokuwa wakisimulia wakimbizi hao, nimesoma maandishi mengi na kuangalia filamu juu ya mauaji ya Rwanda; nilikuwa sijapata picha kamili ya mauaji hayo mpaka juzi tarehe 17.10.2011 nilipotembelea makumbusho ya mauaji ya kimbali.

Makala mbili zilizotangulia, nilielezea safari ya Kigali na sherehe za Kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere. Nilielezea maendeleo ya kasi nchini Rwanda chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Rais Paul Kagame. Wanyarwanda wakikuonyesha maendeleo yao; nyumba za kisasa, usafi wa jiji lao la Kigali na miji mingine, huduma ya maji, shule, hospitali na kukuhakikishia kwamba sasa nchi ina amani na utulivu, watahitimisha ziara kwa kupeleka kwenye makumbusho ya mauaji ya kimbali. Hawawezi kusahau tukio hilo, imebaki kuwa kumbukumbu isiofutika. Wanasamehe yaliyotokea, lakini kamwe hawawezi kusahau. Hivyo nahitimisha makala zangu juu ya safari ya Rwanda, kwa kuandika juu ya Makumbusho ya mauaji ya kimbali. Swali langu kubwa likiwa: Mauaji ya Kimbali Rwanda, nani wa kujifunza.

Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Balozi Dkt. Matiko, alitwambia “ Mwezi wa nne, kila mwaka ni juma zima la kukumbuka ya mauaji ya kimbali. Kila kitu hapa kinakufa ganzi. Hakuna shughuli zinazoendelea. Taifa linakuwa kwenye majonzi makubwa ya kukumbuka ndugu zao waliopoteza maisha yao wakati wa mauaji ya kimbali”.

Rwanda ina vituo vingi vya Makumbusho ya mauaji ya kimbali, sisi tulitembelea vituo viwili, kituo cha Nyamata na Ntarama. Vituo hivi viko kwenye eneo la Bugesera, ambako kulikuwa na Watutsi wengi. Historia ni kwamba baada ya ile vita ya 1959, watawala wa Kihutu waliamua Watutsi wapelekwe Bugesera ili wafe kwa kushambuliwa na mbungo. Walikufa wachache wakati ule, maana walipata mbinu za kupambana na mbungo mpaka mauaji ya kimbali yalipowakuta.

Nyamata, ilikuwa ni parokia ya Kanisa katoliki na Ntarama kilikuwa ni kigango cha parokia ya Nyamata. Ndani ya kanisa la Nyamata, waliuawa watu elfu kumi (10000) na miili ya watu hawa imetunzwa kwenye kanisa hili. Kigango cha Ntarama waliuawa watu elfu tano (5000) na miili ya watu hawa na vitu vyao kama vile nguo, viatu, magodoro, vifaa vya maji bado vinatunzwa kwenye kanisa hili dogo.

Vifaa vilivyotumika kwa mauaji, kama mapanga, nyundo na vijiti walivyokuwa wakiwaingizia wanawake sehemu za siri hadi vinatokea mdomoni, bado vimetunzwa. Damu zilizotapakaa kwenye makanisa hayo bado zinaonekana na hasa sehemu ambapo watoto wadogo walikuwa wakibamizwa hadi vichwa vinapasuka, damu iliyokauka inaonekana kwenye ukuta na kuashiria kwamba watoto wengi walikufa kwa kubamizwa kwenye ukuta.

Makanisa haya mawili hayatumiki tena kwa ibada. Yamebaki kama vituo vya makumbusho ya mauaji ya kimbali. Wamejitahidi kuacha kila kitu kilivyokuwa mwaka 1994, ingawa kwenye kanisa la Nyamata, wamejenga kaburi kubwa chini ya kanisa, kutunzia mabaki ya miili ya wahanga wa mauaji ya kimbali. Pia nje ya kanisa la Nyamata, wamejenga kaburi kubwa ambalo mtu unaweza kuingia na kushuhudia mwenyewe mabaki ya miili ya wahanga wa mauaji ya kimbali.

Mwili wa Mwanamke, aliyebakwa na wanaume 20, na baadaye kuteswa ahadi kufa kwa kuwekewa kijiti sehemu za siri na kutokea mdomoni umetunzwa kwenye kanisa la Nyamata. Mauaji na mateso ya kutisha yalitokea kanisani na kuna ushahidi kwamba watu wengi waliuawa juu ya Altare, meza ambayo kila Jumapili padri wao alikuwa akisimama na kugeuza mkate kuwa mwili wa Bwana, na divai kuwa damu ya Yesu; watu wote wa Nyamata, waliouawa na walioua walikuwa kila Jumapili wakikutana kwenye kanisa hilo kusali pamoja.

Watu walikimbilia kanisa kupata ulinzi. Miaka ya nyuma makanisa ndo yalikuwa kimbilio. Waliamini hakuna baya linaweza kutokea kanisani. Wauaji walitumia mbinu hiyo kuwahadaa Watutsi kukimbilia kanisani, ili wapate njia nzuri ya kutekeleza mauaji yao. Baada ya kuhakikisha idadi kubwa imeingia kanisani, walitoa taarifa kwa jeshi. Hivyo kwa kiasi kikubwa mauaji ya Nyamata na Ntarama, yalifanywa na Jeshi. Mabaki ya risasi na mabomu kwenye kanisa la Nyamata, matundu ya risasi kwenye kuta, milango na paa la kanisa hilo ni ushahidi wa kutosha kwamba mauaji hayo hayakutekelezwa kwa mapanga na nyundo tu bali hata kwa risasi na mabomu.

Risasi hazikuangalia Mwili ya Kristu, maana kwenye kanisa hilo la Nyamata, kisanduku(Tabenakulo) kinachotumika kuhifadhi mwili wa Kristu, kilicharazwa risasi, na ni wazi hostia (Mwili wa Kristu) zilimwagika chini. Bwana Yesu, akawaacha watu wake kuchinjana mbele yake! Sanamu ya Bikira Maria, mama wa shauri jema, mama wa huruma na upendo, kwenye kanisa hilo nayo ilicharazwa risasi! Sanamu hiyo bado ipo hapo kanisani na “majeraha” yake! Hapana shaka kwamba ukatili wa kutisha ulifanywa kwenye kanisa hilo.

Binti anayewapokea wageni na kuwaelezea yaliyotokea hapo Nyamata, alikuwa na umri wa miaka 8 mauaji yalipotokea. Ana kumbukumbu ya mauaji hayo yaliyotekelezwa ndani ya siku mbili tu. Baada ya kututembeza, kutuonyesha masalia ya miili na kutuelezea kwa kirefu yaliyotokea Nyamata, alituuliza swali gumu ambalo hatukupata jibu lake: “ Baada ya kutembelea makumbusho haya, mna ushauri gani? Je ni vizuri kuendelea kuonyesha masalia ya miili ya wahanga wa Mauaji ya kimbali, au tuizike na kufunika kabisa na kuisahau historia hii ya uchungu? Mnatushauri nini ndugu zetu kutoka Tanzania?”

Hakuna jibu lililotoka. Tulitizamana sote na kasha kimya kilitawala. Ni wazi kila mtu alikuwa na jibu lake. Tulipokuwa kwenye gari tukirudi hotelini tulikofikia, mjadala ulianza: wengine walisema “ Ni bora kuifunika miili na kuacha kuonyesha, maana kuionyesha kunaweza kuchochea hasira” wengine na hasa wakereketwa wa “amani” walisema “ isifunikwe ili watu waone na kujifunza kutochezea amani”. Ni imani yangu hata wewe msomaji wa makala hii utakuwa na maoni yako kuhusu jambo hili. Unaweza kutoa maoni yako, Wanyarwanda ni wasikifu, watasikia.

Tulikuwa kama watanzania ishirini na tano tuliotembelea makumbusho haya ya Nyamata na Ntarama. Kila mtu alikuwa na la kwake moyoni. Kilichokuwa wazi ni kwamba simanzi, hofu na huzuni vilimgusa kila mmoja wetu. Kila mmoja wetu alionyesha kuchukizwa na unyama uliotendeka kanisani. Mimi binafsi nilikuwa na maswali mengi kichwani mwangu: Kwa nini mauaji haya yalitokea kanisani? Je, leo hii Kanisa Katoliki la Rwanda lina mbinu gani za kutibu majeraha haya na kama kanisa lina msimamo gani juu ya makumbusho ya mauaji ya kimbali ambayo yako kwenye makanisa yao? Wana nguvu za kuweza kusimama na kuhubiri? Je kwa nini roho ya mtu igeuke na kuwa kama ya mnyama? Haingii akilini kwamba vitendo vya Nyamata na Ntarama vilitendwa na binadamu. Kwa nini watu walifikia hatua hiyo? Ni propaganda za kisiasa? Ni siasa mbaya? Ni uongozi na utawala mbovu ni nini?

Tulielezwa kwamba kwenye makanisa mengine yalikotokea mauaji, hata mapadri walishiriki mauaji. Waliwatenga Wanyarwanda kwenye makundi ya Wahutu na Watutsi, na kuwaruhusu wanajeshi kuwaua Watutsi. Baadhi ya mapadri hawa bado wanaishi na kuhubiri neno la Mungu Rwanda. Na la kushangaza ni kwamba makanisa yanajaa waumini, nilipouliza, niliambiwa “ Wanyarwanda wanapenda sana dini”

Wakati mimi nikitafakari ya kwangu na wenzangu walikuwa wakitafakari pia. Huwezi kutembelea Nyamata au vituo vingine vya mauaji ya kimbali ukatoka bila tafakuri nzito. Wenzetu wengine ilibidi wameze vidonge vya kuteremsha shinikizo la damu na wengine niliona wakimeza panadol kutuliza maumivu ya kichwa baada ya kushuhudia unyama unaoweza kutendwa na binadamu. Baadhi ya wenzetu walisikika wakisema kwa masikitiko “ Watanzania wenzetu wasiopenda amani, waje hapa Nyamata na Ntarama wajifunze”.

Swali langu kwao likawa “ Ni watanzania gani wasiopenda amani”. Jibu likawa “ Wale wanaopenda maandamano”.

Nafikiri tusijidanganye. Mauaji ya kimbali ya Rwanda, ni fundisho letu sote. Ni fundisho kwa chama tawala cha CCM na ni fundisho kwa wapinzani pia. Ni lazima kutambua kwamba binadamu ni binadamu, awe CCM au upinzani anabaki kuwa yule yule; mwenye tamaa, mwenye wivu, mwenye kiburi, mwenye ubaguzi, mwenye mashindano, mwenye kutaka madaraka, mwenye kutaka kuwanyanyasa wengine, mwenye kutaka kuwa bora zaidi ya wengine. Hivyo mwanadamu ni lazima aongozwe na vitu kama sheria, katiba, kanuni, utamaduni, mila na desturi. Na haya ni lazima kuyajenga pamoja kama taifa na kila mtu lazima awe na mchango wake na ni lazima kila mtu kuyafuata na kuyaheshimu. Nchi si mali ya mtu au kikundi chochote cha kisiasa. Ni imani yangu kwamba hakuna mtu asiyependa Amani. Sote tunapenda amani, ndo maana ninasema ni jambo muhimu sote kujifunza matokeo ya uvunjifu wa amani kutoka Rwanda.

Matukio ya Igunga, ya wanasiasa kupanda jukwaani na bastola, si kupenda amani! Kununua shahada za watu ili  wasipige kura si kupenda amani, maana watu hawa wakitaka kupiga kura kwa nguvu, amani itapotea. Serikali kuingiza nchi kwenye mikataba mibovu, si kupenda amani, maana kuna siku wananchi watasimama na kuikataa mikataba hii, na hili likitokea hakuna amani. Kupora ardhi kwa visingizio vya uwekezaji si kupenda amani, maana wananchi wakisimama kudai ardhi yao amani itapotea.

Tusipokuwa na chakula cha kutosha, amani itapotea! Mtu mwenye njaa hawezi kuwa na amani. Bidhaa muhimu zinapanda bei usiku na mchana; mafuta ya taa yanapanda bei, sukari inapanda bei na vyakula sasa vinapanda bei. Hatuwezi kuwa na amani , kama wananchi watakuwa hawana bidhaa muhimu katika maisha yao ya kila siku. Amani itavunjika pole pole na hatimaye inaweza kufikia kilele kama kile cha Nyamata.

Tusiwatupie lawama  wale wanaopenda maandamano. Tujiangalie kama taifa tunaelekea wapi? Tunajenga taifa la kuvunja amani siku za mbele au tunaweka misingi imara ya kulinda amani na utulivu? Tumeanza kujenga matabaka ya walionacho na wasiokuwa nacho, ufa unakuwa mkubwa kila kukicha. Tunajenga sekondari za kata na kuacha watoto wa vigogo kusoma shule nzuri na nje ya nchi. Je watoto hawa kesho na keshokutwa watapikika chungu kimoja? Hatuna mpango mzuri wa kuwaingiza kwenye jamii watoto wa mitaani. Tunawaacha wanakulia mitaani, wanaoa na kuolewa na kutengeneza familia wakiwa mitaani. Siku ya siku hawa watakuwa salama yetu?

Tusipoziba ufa tutajenga ukuta! Tusikwepe wajibu wetu, kujenga amani ni kazi yetu sote. Kama kuna la kujifunza juu ya kuilinda amani ni lazima tujifunze wote. Kwa maana hiyo mauaji ya kimbali ya Rwanda ni fundisho kwa watanzania wote.

Na,
Padri Privatus Karugendo.

+255 754 6331 22.
KAMA CHADEMA HAWANA “GOOD WILL” MWENYE “GOOD WILL” NI NANI?

Tarehe 10 Novemba wakati Waziri Mkuu Pinda akijibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa Wabunge, alisema kwamba CHADEMA hawana “Good will”. Waziri Mkuu alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, aliyetaka kujua hatua zilizochukuliwa na serikali kumaliza mgogoro wa Arusha:

“Nyie Chadema hicho mnachokifanya huko Arusha hakionyeshi nia njema ya kisiasa ya kumaliza mgogoro huo, huu uwanaharakati wa ‘Peoples Power’ wala hauna tija”.

Waziri Mkuu aliendelea kusisitiza kwamba misuguano ya kisiasa kule Arusha na kwingineko inahitaji “Good will” kwa pande zote. Kwa maana kwamba Serikali iwe na “Good will”, CCM wawe na “Good will” na Chadema wawe na “Good will”. Bahati mbaya alishindwa kuonyesha kwa mifano “Good will” ya upande mwingine zaidi ya kukilaumu chama cha Chadema kwamba hakina  “Good will”. Tungependa na kusikia juu ya “Good will”  ya serikali na ya CCM.

Nimekuwa na heshima kubwa kwa Waziri Mkuu, nimekuwa nikiamini na naendelea kuamini kwamba ni mtu makini. Kwamba sifa anayopewa ya Mtoto wa Mkulima ni kweli, maana hana makuu na wala jina lake halisikiki kwa watu waliohujumu rasilimali za taifa letu. Ni mtu ambaye jina lake halikutajwa huko nyuma kwa watu waliokuwa wakitafuta kuingia madarakani kwa njia zozote zile. Nimekuwa nikimchukulia kuwa mzalendo na mtu mwenye mapenzi makubwa kwa Tanzania na watu wake. Lakini kwa hili la “Good will” amenikwaza! Amenifanya niwe na mashaka kama anafahamu maana ya neno “Good will” kwa lugha yetu “Nia njema”. Najiuliza maswali mengi bila majibu. “Nia njema” ni mtu kuwa mjinga, kukaa kimya na kukubali kila kitu hata kama inamaanisha kupoteza maisha yako, ya familia yako, ya taifa lako na maisha ya vizazi vijavyo? Kupinga malipo ya Dowans, ni kutokuwa na “Good will”, kutaka Demokrasia ya kweli, bila kutumia fedha kununua kura na shahada ni kutokuwa na “Good will”? Kudai rasilimali za nchi hii ziwanufaishe watanzania wote ni kutokuwa na “Good will”? Kutaka watanzania wote kushiriki mjadala wa kuandika katiba mpya ni kutokuwa na “Good will”? Kupinga matumizi mabaya ya fedha za umma na uporwaji wa ardhi unaoendelea katika taifa letu ni kutokuwa na “Good will”?

Mtu mwenye “Good will” ni lazima apende majadiliano na kutafuta muafaka.  Mtu mwenye “Good will” ni lazima atambue kwamba Tanzania ni yetu sote na vyama vyote vya siasa ni sawa. Waziri Mkuu Pinda, anatoa ushuhuda kwamba Chadema, kwa suala la Arusha walikuwa tayari kukaa meza moja na CCM kujadiliana, lakini CCM hawakuona kama kuna jambo la kujadiliana na CHADEMA. Mtu anayeijua hali ya Arusha, atasema hakuna la kujadiliana? Mheshimiwa Waziri Mkuu, alisema hivi Bungeni:
 “Sasa baada ya hapo niliona barua ya CCM kwenda kwa msajili, ambayo wanasema hawaoni kama kuna jambo la kuzungumza na Chadema. Labda kwa wenzetu kama wanaona liko jambo bado la kuzungumza walete taarifa”.

Kwa maelezo haya ya Waziri Mkuu, ambaye ndiye aliyetoa ushauri wa Msajili wa vyama vya siasa kuwakutanisha Chadema na CCM, ili wajadiliane tofauti zao kwenye Umeya wa Arusha, inayonyesha kwamba CCM ndo walikataa kukaa meza moja na Chadema. Hapa nani hana “Good will”, sitaki kuamini kwamba Waziri Mkuu, alitumia neno hili bila kulijua maana yake, au kwamba mapenzi ya chama chake yamemlewesha kiasi cha kutotambua mema na mabaya.

Waziri Mkuu anasema: “Labda kwa wenzetu kama wanaona liko jambo bado la kuzungumza walete taarifa”. Kama CCM, hawako tayari kukaa meza moja na CHADEMA kupatanishwa kwa suala la Arusha, hivyo  taarifa anayosema waziri Mkuu ipelekwe wapi na kwa njia zipi? Ndo hivyo inapelekwa kwa njia ya maandamano. Duniani kote, serikali zinazoziba masikio na kuwa na kiburi kupindukia kama ilivyo serikali ya CCM, zinapelekewa ujumbe kwa maandamano na migomo.

Mtu anayeamua kufanya maandamano, au mtu anayeamua kuvaa mabomu na kujilipua, maana yake ni kwamba njia nyingine za kudai haki zake na za wengine zimeshindikana. Uchaguzi wa umeya wa Arusha, ulivurugwa makusudi mazima na CCM kwa kushirikiana na vyombo vya dola. Chadema wangefanya nini zaidi? Wangefanya nini kuonyesha kwamba wana “Good will”? Kukaa kimya na kutulia wakishuhudia haki ikipotea ndiyo kuwa na “Good will”?

Ni nani mwenye “Good will” katika taifa letu la Tanzania? Haya yote tunayoyashuhudia ambayo yamekuwa kama Litania ya EPA, DOWANS, RICHMOND na mengine mengi ndo “Good will”? Thamani ya shilingi inashuka kwa kasi, bei ya mafuta inapanda, bei za  bidhaa nyingine muhimu kama sukari inapanda kwa kasi, mishahara ya watumishi inachelewa…. Hapa kuna “Good will”?

Tumeshuhudia jinsi wabunge wa upinzani walivyo na mchango chanya ndani ya Bunge letu Tukufu. Lakini mara nyingi hoja zao zinatupwa kwa sababu ya wingi wa wabunge wa CCM. “Good will” iko wapi kama wabunge wa CCM, wanazikataa hoja za CHADEMA si kwa kutokuwa na mantiki, bali kwa vile zimetoka upinzani?

Ningependa kuuliza swali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu: Mambo yanapokwenda ovyo serikalini, yeye anajua fika kwamba kuna mambo mengi yanakwenda ovyo. Analikumbuka sakata la Jairo, wapinzani ambao kazi yao kubwa ni kuisahihisha serikali na kuiondoa madarakani (kwa kura) kama haiwezi kutimiza mahitaji ya watanzania ,wafanye nini mambo yanapokwenda ovyo? Wakae kimya ili kuonyesha wana “Good will”?

“Good will” ni kuunga mkono kila kitu hata mambo ya ovyo? Inashangaza kwenye mjadala unaoendelea wa Sheria ya Manunuzi ya Umma, wabunge wa CCM, wanaunga mkono Serikali kununua vitu vichakavu. Kisingizio kwamba hatuwezi kununua vitu vipya, maana hatuna fedha. Ni kweli hatuna fedha?  Nchi yenye dhahabu, almasi, na madini mengine mengi, nchi yenye utajiri mwingine wa mbuga za wanyama, maziwa yenye samaki na ardhi kubwa kwa kilimo, tunasema hatuna fedha? Kama tunakubali kununua vitu vichakavu, basi na viongozi wetu wasitibiwe tena nje ya nchi. Tukubali kwamba sisi ni masikini na hadhi yetu ni vitu chakavu. Viongozi wetu wanazikimbia hospitali zetu na kwenda nchi za nje, kwa vile hospitali zetu ni chakavu. Zingekuwa nzuri na ziko kwenye viwango vizuri wangetibiwa hapa.

“Good will” iko wapi? Watanzania wanalilia katiba mpya. Lakini mswada unaopelekwa Bungeni ni wa marekebisho ya katiba. Kurekebisha katiba na kuandika katiba mpya, ni vitu viwili tofauti. Watu wakiingia barabarani kudai “Katiba mpya” tutasema hawana “Good will”?

Juzi hapa Umoja wa Vijana wa CCM, walikatazwa kufanya mkutano na maandamano, hawakusikia. Wakafanya na hakuna kilichotokea. Chadema, wakijaribu wanakamatwa na kuwekwa ndani. “Good will” iko wapi, kama sheria zinafanya kazi kwa upande mmoja tu wa wapinzani na kukaa kimya kwa upande mwingine wa chama tawala?

Kuna mifano mingi inayoonesha jinsi serikali inavyonyanyasa upinzani na kukipendelea chama tawala. Sina haja ya kutoa mifano maana sote tunaishi Tanzania na tunashuhudia yale yanayotokea kila siku. Kama tuna nia njema na taifa letu, tuondokane na “Kiburi” cha kisiasa, tushirikiane kulijenga taifa letu.

Na,
Padri Privatus Karugendo.

WAHAMIAJI HARAMU, TUNA MPANGO WA KUDUMU?

Tanzania inapakana na nchi nyingi, hivyo suala la kuwa na wahamiaji haramu si la kushangaza. Na hapa ni lazima tutofautishe “Uhamiaji haramu” wa kihistoria na ule ulioibuka siku za hivi karibuni wa watu kutoka nchi za Somalia na Ethiopia wanaopitia Tanzania wakielekea Afrika ya Kusini kutafuta kazi. Hili ni wimbi jipya, mipango yao ikikwama wanajikuta wakiishi Tanzania kinyume na sheria. Binafsi nimeandika sana juu ya suala hili la wahamiaji haramu wa kihistoria  na wachambuzi wengine wamelielezea mara kwa mara, lakini kwa vile kuna dalili za suala hili kutoeleweka vizuri miongoni mwa watanzania  na hasa viongozi wetu kama vile wabunge ni vyema kulijadili tena na kutafuta njia ya kuwa na mpango wa kudumu kuhusu suala hili.

Ni muhimu sana kwa wabunge wetu ambao ndio wawakilishi wa wananchi, ambao ndio wanaotunga sheria za nchi kuifahamu vizuri historia ya taifa letu, kufahamu vizuri mazingira ya majimbo yao ya uwakilishi na kuyafahamu vizuri mahitaji ya siku kwa siku ya wapiga kura wao. Inapotokea mbunge akaonyesha dalili za kutofahamu mahitaji muhimu ya watu wake, inatia simanzi na  ni hatari kubwa. Kwa mbunge aliye makini, kinachotangulia si chama chake cha siasa na wala si serikali iliyo madarakani, bali ni wananchi wake waliomchagua na kumtuma awawakilishe Bungeni.

Ukiachia mbali historia ya bara letu la Afrika ya mipaka ya nchi zetu kuibuka 1884? Mwalimu Nyerere, alifungua mipaka ya nchi yetu kwa Waafrika wote. Tanzania, iliwapokea wakimbizi na wapigania uhuru. Kwa miaka mingi Tanzania, ilikuwa ni kimbilio la wengi na msamiati huu wa “Wahamiaji haramu” haukujulikana. Kwa njia hii watu wengi wa nchi jirani walipata uraia wa Tanzania na wengine waliendelea kuishi hivyo hivyo bila hata kujishughulisha kuomba uraia. Kwa maana nyingine, huko nyuma hakukuwa na mpango wa kudumu wa kulishughulikia suala la wahamiaji haramu.. au hakukuwa na umuhimu wa kutengeneza mpango wa kulishughulikia suala hili.

Leo hii tunahitaji mpango huu wa kudumu. Tunahitaji kuwatambua wahamiaji haramu na kuwatungia sheria na mpangilio wa kuendelea kuishi hapa Tanzania. Busara si kuwafukuza, maana kuna wahamiaji haramu wanaoweza kuishi hapa Tanzania kama wawekezaji; wanaweza kutoa kodi na kuchangia  pato la taifa. Inawezekana kabisa kukaa kwao ndani ya nchi bila kibali, ni makosa yetu kama taifa kutokuwa na mpango wa kudumu kuhusu suala zima la wahamiaji haramu. Hivyo badala ya kelele za wabunge juu ya wahamiaji haramu, tunataka kusikia wakijadili mchakato wa kuanzisha mpango wa kudumu juu ya wahamiaji haramu na sheria ya kusimamia mpango huu. Hayo ndiyo mambo ya kujadiliwa na wabunge makini, si kulalamika bali ni kutafuta majibu na kupanga mipango ya kusonga mbele.

Tanzania, tunaelekea kusherehekea miaka 50 ya uhuru wetu bila kuwa na vitambulisho vya uraia. Mchakato wa vitambulisho hivi uko mbioni, lakini hatuwezi kuwa navyo kabla ya sherehe za miaka 50 ya uhuru wetu. Zoezi hili likianza tunaweza kushuhudia idadi kubwa ya watu ambao ni wahamiaji haramu. Hata ikitokea hivyo, zoezi zima liendeshwe kwa misingi ya utu na roho ili aliyoipandikiza Mwalimu Nyerere ya Umajumui wa Afrika. Watu wasiwekwe ndani, wasinyang’anywe mali zao na kurudishwa kwa nguvu kwenye nchi zao za asili.

Kama nilivyosema mwanzoni mwa makala hii, ni kwamba Tanzania inapakana na nchi nyingi, hivyo mikoa mingi ina tatizo hili la wahamiaji haramu, lakini tatizo hili ni kubwa zaidi katika Mkoa wa Kagera. Ni vigumu kuelewa ni kwa nini tatizo hili linasikika sana Kagera, kuliko kwingine. Mfano Mtwara, watu wa Msumbiji wanaingia na kutoka na wengine wanaishi Tanzania bila kelele za “Uhamiaji haramu”. Arusha ndugu zangu Wamasai wanaingia Kenya na kurudi Tanzania na kuishi bila kuitambua mipaka ya nchi hizi mbili, lakini hakuna kelele za “Uhamiaji haramu”. Juzi bungeni suala la wahamiaji haramu katika mkoa wa Kagera, liliibuka tena. Naibu Waziri wa  Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Benedict Ole Nangolo, alionyesha kulifahamu vizuri suala hili na kutoa jibu kwamba suala hili linahitaji “ Ushirikishwaji mkubwa”.

Jibu la Benedict Ole Nangolo, linaonyesha umakini mkubwa, ni aina ya wabunge tunaowahitaji kuliendeleza taifa letu ni aina ya wabunge wanaoguswa na maisha ya wananchi ni kinyume na mawazo ya viongozi wengine wanaofikiri jibu la tatizo la wahamiaji haramu ni kuwafukuza na kuwarudisha makwao. Kama nilimwelewa vizuri Mheshimiwa Benedict Ole Nangolo, ni kwamba suala hili la wahamiaji haramu linahitaji mpango wa kudumu. Mpango ambao chombo pekee cha kuutengeneza ni Bunge letu tukufu.

Kwa faida ya msomaji wa makala hii ni kwamba Mkoa wa Kagera unapakana na nchi tatu. Uganda, Rwanda na Burundi. Na kuna historia ya miaka mingi ya watu wa nchi hizi kuingiliana, kuwa na utamaduni unaofanana na lugha zinazofanana. Mipaka ya nchi hizi haikufanikiwa kuondoa udugu ulioanzishwa na mababu zetu. Nakumbuka kuandika makala Fulani nikisema kwamba mwenyeji wa Mkoa wa Kagera ambaye hana chimbuko Rwanda, Burundi au Uganda si mzaliwa wa mkoa huo! Kwa hiyo mbali na wakimbizi kuna wahamiaji wa aina nyingi mkoani Kagera, kuna wale wanaovuka mpaka kuja kusalimia ndugu na jamaa na wakinogewa wanahamia, kuna wakimbizi wa kisiasa na wakimbizi wa njaa wanaovuka mpaka kutafuta ardhi yenye rutuba lakini wanao lalamikiwa sana ni wale wahamiaji wafugaji. Hata juzi bungeni Mbunge wa Karagwe, alikuwa akiwalalamikia wahamiaji haramu wafugaji.

Hawa wahamiaji haramu wafugaji wanajulikana kama Wahima. Ni wafugaji kama vile Wamasai na wasukuma. Wanahama kutoka sehemu moja hadi nyingine kutafuta malisho ya mifugo. Wahima, kama walivyo Wamasai hawatambui mipaka ya nchi, kwao mifugo ni muhimu zaidi ya kila kitu. Mifugo ni muhimu kuliko mipaka ya nchi na kuliko vitambulisho vya uraia. Na kawaida hawana utamaduni wa kumiliki ardhi, wao wanatafuta malisho ya mifugo. Daima wanahama kutafuta maeneo mazuri ya kulisha mifugo yao. Magonjwa yakishambulia mifugo yao ikafa, ni lazima wahame kwenye maeneo hayo. Hawajengi nyumba za kudumu, na kwa maana hiyo hawana makazi ya kudumu!

Wahima, ni kabila ambalo limeishi miaka mingi katika maeneo ya maziwa makuu. Wamekuwa wakihama kutoka eneo moja hadi jingine wakitafuta malisho ya mifugo yao. Mipaka ya wakoloni ndo iliwatenganisha Wahima wa Burundi, Wahima wa Rwanda, Wahima wa Uganda na Wahima wa Tanzania. Hata hivyo Wahima hawa wamekuwa wakivuka mipaka ya nchi hizi bila kujali vitambulisho wakiwa katika harakati zao za kutafuta malisho.

Kwa maana hii basi, Wahima wamekuwa wakitoka Uganda, Rwanda na Burundi na kuja Tanzania kutafuta malisho ya mifugo yao. Lakini kuna wahima ambao wamekuwa wakiishi Tanzania miaka yote. Wanazunguka wilaya za Mkoa wa Kagera, bila kuvuka mipaka ya nchi. Mkoa wa Kagera unazalisha maziwa mengi na nyama kutokana na wafugaji hawa wahima.

Tanzania ilipoingiliwa na kirusi cha “wahamiaji haramu”, wahima wote bila kujali wale ambao ni watanzania, wamekuwa wakisumbuliwa. Wanakamatwa na kuwekwa ndani, wananyang’anywa mifugo yao na wakati mwingine wanasombwa na kupelekwa Rwanda. Kwa vile hadi leo hii hatuna vitambulisho vya uraia, mkoani Kagera, sura za watu zimekuwa zikitumika kama vitambulisho!
Kwa sura wahima wanafanana na Watutsi. Bila vitambulisho na mpango wa kudumu juu ya wahamiaji haramu, wahima wote watachukuliwa kuwa ni wahamiaji haramu. Wilaya ya Karagwe, ambayo ina wahima wengi, imekuwa ikitajwa kuongoza kwa kuwa na “Wahamiaji haramu”. Ukweli ni kwamba baadhi ya “Wahamiaji haramu” hawa ni wahima na kufuatana na mipaka ya kikoloni ya 1884? Hawa ni watanzania!

Hawa wahima wa Karagwe, wamesumbuliwa sana. Baadhi yao wamefungwa mara nyingi na kutozwa “hongo” ya ng’ombe. Kwa kutotaka usumbufu, wahima hawa wamekuwa wakitoa ng’ombe na fedha kwa viongozi wa serikali na wafanyakazi wa Uhamiaji ili wasikamatwe na kupelekwa Rwanda. Hata hivyo kuna baadhi waliokumbwa na zoezi hili la kupelekwa Rwanda. Walinyang’anywa mifugo yao, kwa maneno mengine walinyang’anywa maisha yao na kupelekwa ugenini Rwanda.

Serikali ya Rwanda, inalitambua tatizo hili la Wahima, na inaamini suluhu si kuwasomba wahima na kuwapeleka Rwanda, bali ni kutunga sera na sheria juu ya watu hawa wafugaji. Wanavyohama hama wakiwa Tanzania, ndivyo watakavyo hama hama wakiwa Rwanda, Burundi au Uganda. Jibu si kuwasomba na kuwapeleka Rwanda nchi inayodhaniwa kuwa ni asili yao, bali ni kuwajengea watu hawa mazingira ya kuishi na kuendesha ufugaji wa kisasa. Kwa vile maisha yao ni mifugo kuna hitaji la kuhakikisha wanaendeleza maisha yao hayo kwa njia za kisasa bila kuvunja sheria za nchi husika. Rwanda, imeanza kuwafundisha wafugaji kwamba kufuga si lazima kuwa na mifugo wengi kiasi cha kulazimika kuhama hama kutafuta malisho, bali ni kuwa na mifugo kiasi na kuitunza vizuri. Mapato yanayotokana na mifugo michache iliyotunzwa vizuri ni makubwa kulinganisha na mifugo mingi isiyotunzwa vizuri. Hili linaweza kuwashawishi wafugaji kuachana na utamaduni wa kuhama hama kutafuta malisho.

Kuna haja kubwa ya kuwa na mpango wa kudumu juu ya jamii hii ya Wahima. Kama ilivyo muhimu pia kuwa na mpango wa kudumu juu ya Wamasai wa Kenya na Tanzania na wasukuma wanaohama kutoka mkoa moja hadi mwingine wakitafuta malisho ya mifugo yao kiasi cha kuvuka hata mipaka ya nchi. Kule Sumbawanga, kuna habari kwamba wasukuma wameanza kuvuka na kuingia nchi jirani.

Nchi za Rwanda, Burundi, Uganda na Tanzania, zikae pamoja na kutunga sheria ya Wahima. Watu hawa waruhusiwe kuzunguka popote kwenye nchi hizi, mradi wasivunje sheria za nchi husika. Watu hawa wajulikane, wapatiwe vitambulisho maalum na kuruhusiwa kuendelea na maisha yao ya ufugaji. Tunapoelekea kwenye ushirikiano wa Jumuiya ya nchi za Afrika ya Mashariki, jambo hili la kuwatambua wahima kama jamii ya watu wanaohama hama kutafuta malisho ya mifugo yao ni muhimu sana. Kuendelea kuwachukulia wahima kuwa ni wahamiaji haramu ni kuwakosea haki yao ya msingi.

Na,
Padri Privatus Karugendo.
+255 754 633122

MIAKA HAMSINI YA UHURU WETU NI HISTORIA YA WATANZANIA WOTE.

Tunaposherehekea miaka hamsini ya uhuru wetu ni wakati mzuri wa kuwakumbuka mashujaa waliopigania uhuru wa taifa letu na ni muhimu pia kuwakumbuka wale wote waliochangia maendeleo ya taifa letu mara baada ya uhuru hadi leo hii. Kumekuwepo na michango mingi ya watu binafsi, mashirika ya dini na mashirika yasiyokuwa kiserikali. Wote hao wamekuwa wakichangia kuijenga Tanzania yetu. Kwa maana hiyo basi historia hii ya miaka hamsini ya uhuru wetu ni mradi wa pamoja uliotekelezwa na watanzania wote na utaendelea kutekelezwa na watanzania wote miaka mingine hamsini na kuendelea.

Ingawa uhuru wetu ni mradi wa pamoja ni vyema kutambua mchango wa makundi mbali mbali. Katika makala hii na nyingine zitakazofuata nitajadili mchango wa harakati wa mashirika yanayotetea usawa wa jinsia na ukombozi wa wanawake kimapinduzi katika kipindi cha miaka hamsini ya uhuru wetu.

Mashirika haya yamefanya mambo mengi ya kutetea haki za binadamu, usawa wa jinsia na ukombozi wa mwanamke kama tutakavyoshuhudia kwenye makala hizi: Mfano kusaidia kuiweka sahihi historia ya taifa letu. Tumekuwa tukisikia majina ya wanaume bila kutajwa wanawake katika historia ya kupigania uhuru wa taifa letu lakini kwa kazi iliyofanywa na TGNP ( Mtandao wa Jinsia Tanzania) wa kutafsiri katika lugha ya Kiswahili utafiti wa Susan Geiger juu ya Wanawake wa TANU, na kuhakikisha kitabu hiki kinasambazwa na kusomwa na wengi, kumeleta mwanga mpya wa ukweli wa Wanawake kushiriki kikamilifu katika kupigania uhuru wa taifa letu. Huu ni mchango mkubwa wa TGNP ambao inawezekana hata na wao hawautambui maana daima tunaelekeza nguvu zetu kwa mambo makubwa ya dunia hii na kusahau maisha ya siku kwa siku yanayotuzunguka. Baada ya uhuru mfumo dume ulishika hatamu, historia ya wanawake waliopigania uhuru ikasahaulika na kufunikwa.

Marehemu Susan Geiger ni msomi mwanaharakati ambaye alifundisha masomo ya Kiafrika na yale ya Jinsia katika Chuo Kikuu cha Minnesota/Twin Cities, huko Marekani kwa muda wa miaka mingi. Alikuja Tanzania kwa mara ya kwanza akiwa mwalimu wa kujitolea katika miaka ya 1960. Baadaye aliendelea kurudi katika nyakati tofauti katika kipindi chote cha maisha yake.

Kazi yake kubwa ya utafiti ilikuwa juu ya historia ya uchifu wa Wachagga. Utafiti huo ndio uliokuwa chimbuko la kujipatia Shahada ya Udaktari wa Falsafa. Baada ya hapo alifanya utafiti mwingine wa makusanyo ya wanawake wanaharakati wapigania uhuru. Susan alikuwa mwanaharakati aliyejitolea kwa michango ya hali na mali hadi mwisho wa maisha yake. Alitoa mchango mkubwa kwa wanamtandao wa masuala ya jinsia hapa nchini ili waweze kuendeleza shughuli zao.

Utafiti wake juu ya Wanawake wa TANU, uliibua mengi yaliyokuwa yamefunikwa. Mbali na Bibi Titi Mohamed, mwanamke anayetajwa kwa mbali katika harakati za kupigania uhuru wa taifa letu, kuna majina ya wanawake wengi waliojulikana kama “Wanawake wa TANU” waliopigana kufa na kupona kulikomboa taifa letu. Kufuatana na ushuhuda wa Wanawake wa TANU, ni kwamba chama hiki kilisimikwa na Wanawake, kama alivyonukuliwa Bi Mashavu binti Kabonge kutoka Tabora:
Nikwambie ukweli, wanawake ndio walioleta TANU. Ukweli ni kwamba wanawake ndio waliofanya hivyo. Wanaume wengi waliogopa kufukuzwa kazi. Waliambiwa na waajiri wao kwamba yeyote atakayejiunga na TANU atafukuzwa mara moja…. Lakini wanawake walikuwa mashabiki wa nguvu wa TANu na wengine waliachika kwa sababu ya sushuli zao za siasa”

Mashavu binti Kabonge, ni kati ya wanaharakati wanawake wa Dar-es-Salaam, waliopigana kufa na kupona kuleta uhuru wa taifa letu, lakini hawatajwi wala kukumbukwa. Hivyo tunaposherehekea miaka hamsini ya uhuru wetu kwa vile TGNP imetusaidia kuyafufua baadhi ya majina ya wapigani uhuru hawa ni bora kuwakumbuka na kuwaenzi. Pia ni wakati kuendeleza mapambo ya mfumo dume ambao ni hatari kwa mambo mengi hadi kuifuta historia. Ni wazi majina ya wanawake hawa waliopigania uhuru wa taifa letu yamefunikwa na mfumo dume! Hakuna maelezo mengine!

Mbali na Mashavu binti Kabonge, kuna majina mengine mengi ya wanaharakati wanawake wa Dar-es-Salaam: Tatu Binti Mzee, pamoja na Bibi Titi Mohamed,Tatu Binti Mzee alikuwa mmoja wa wajumbe wanawake wa kwanza katika chombo muhimu cha maamuzi, yaani, kamati Kuu ya Chama.

Halima Hamisi, huyu naye ni mpambanaji wa kuleta uhuru, katika utafiti wa Susan, ananukuliwa akisema “ Tulitembea kwa miguu siku nzima bila chakula. Ukichukua chai nyumbani na ukijaliwa kupata karanga, unanunua. Wakati mwingine tuliweza kupata fedha za chakula kutoka ofisi ya TANU, lakini ilibidi  wapige hesabu kwa makini….”

Wanawake wengine wa Dar-es-Salaam, walioshiriki harakati za kuleta uhuru na majina yao yamefunikwa na historia ni: Salima Ferouz, Binti Kipara, Mwasaburi Ali, Fatuma Abdallah na wengine wengi ambao watafufuliwa na  tafiti nyingine zitakazofanyika kwa kuchochewa na hii ya Susan.

Katika utafiti wa Susan, Salima Ferouz, ananukuliwa akisema: “ Sisi wanawake tulikuwa na nguvu… tuliongoza njia kwa sababu ya uonevu wa watoto wetu na jinsi tulivyowekwa ndani… tulifanya kazi pamoja, tukajiunga na Kitengo cha wanawake na kutumikia TANU, tukichangisha fedha na kuwahamasisha wengine wengi wajiunge..”

Hata mikoani kulikuwa na wanawake walioshiriki harakati za ukombozi wa taifa letu. Kule Kilimanjaro kulikuwa na Halima Selengia Kinabo, Mwamvita Salim, Zainab Hatibu, Morio Kinabo, Violet Njiro, Elizabeth Gupta, Kanasia Tade Mtenga,Natujwa Daniel Mashamba na Lucy Lameck.

Hata kule Mwanza kulikuwa na wanaharakati wanawake waliopigania uhuru wa taifa letu, lakini historia haiwakumbuki  tena. Wanawake hao ni: Agnes Sahani, Aziza Lucas, Tunu Nyembo, Halima Ntungi, Mwajuma Msafiri, Pili Juma, Mwamvua Kibonge, Zuhura Mussa  na  Chausiku Mzee.

Ni wazi wako wanawake wengine wengi walioshiriki harakati za kuleta uhuru wa taifa letu, ni kazi ya Mashirika yanayotetea usawa wa jinsia na ukombozi wa mwanamke kwa kushirikiana na watanzania wanaopenda kuweka kumbukumbu sahihi kuendeleza utafiti na kuibua majina mengine ya wanaharakati wote walioshiriki kuleta uhuru wa taifa letu. Tusitake kusherehekea kwa kuimba, kunywa na kucheza bila kuiandika historia sahihi ya taifa letu.

Ni lazima tujiulize tumeteleza wapi? Kama  huko nyuma tuliweza kuendesha harambee ya kuchangia harakati za mapambano, shughuli zote zikaendelea bila misaada ya kutoka nje. Mapato yote ya nchi yakiwa mikononi mwa mkoloni. Inakuwaje sasa wakati tumeshika mapato ya nchi mikononi mwetu, tunaendelea kuomba misaada ya kujenga vyoo na vyandarua? Uwezo wa kujitegemea uliokuwa miongoni mwa wananchi wakati wa kupigania uhuru umekwenda wapi? Tulipigania uhuru wa kisiasa, ili  tupoteze uhuru wa kujitegemea na kujiamulia mambo yetu wenyewe? Ukipokea misaada, ni vigumu kukwepa masharti yake!

Makala hii ni mwanzo mzuri wa kuangalia mchango wa Mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayoshughulikia usawa wa jinsia na ukombozi wa mwanamke. Swali la kujiuliza ni je, kama Wanawake walikuwa mstari wa mbele wakati wa kupigania uhuru wetu, ilitokea nini wakawa mstari wa nyuma baada ya uhuru? Wanawake walichangisha fedha za kuendesha mapambano, walifanya kazi kwa nguvu kupata fedha, walipika maandazi na wengine walifanya kazi za kujidhalilisha ili wapate fedha za kukiendesha chama cha TANU. Mapambano ya kuleta uhuru hayakutegemea misaada kutoka nje. Uwezo mkubwa wa kujitegemea ulioongozwa na wanawake ulikwenda wapi baada ya uhuru kufikia hatua ya kutafuta fedha kutoka nje ili kuendesha “ Miradi” ya kuwakomboa wanawake wa taifa letu? Ni lazima kutafakari kwa kina wakati tukisherehekea miaka Hamsini ya taifa letu.

Na,
Padri Privatus Karugendo.
UTETEZI WA JINSIA NA UKOMBOZI WA WANAWAKE KIMAPINDUZI NDANI YA MIAKA HAMSINI YA UHURU WETU.

TGNP,FEMACT  na mashirika mengine yanayoshughulika na utetezi wa jinsia na ukombozi wa mwanamke kimapinduzi wanatukaribisha kutafakari pamoja juu ya mchango wao na changamoto walizokumbana nazo ndani ya miaka hamsini ya uhuru wetu. Mashirika mengi ya kutetea Jinsia na ukombozi wa mwanamke kimapinduzi yameanzishwa baada ya Beijing. Hivyo yaliyo mengi yanatekeleza maamuzi ya mkutano huo wa Beijing. Kwa namna moja ama nyingine tunapozunguzia mchango wa mashirika haya ni kutaka kujua mafanikio na changamoto ya kutekeleza maazimio ya Beijing. Kwa upande mmoja mawazo haya ni sahihi kabisa, lakini kwa upande wa historia ya Tanzania, harakati za kijinsia na ukombozi wa mwanamke zinakwenda nyuma hadi kwenye kupigania uhuru wetu.

Tulipigana kwa pamoja kumwondoa mkoloni na kushindwa kufuta kabisa vikaragosi vya ukoloni. Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanajaribu kupambana na vikaragosi vya ukoloni. Mfumo wa Soko huria na nguvu za kutisha za ubeberu vinatufanya kuwa na “Uhuru” wa bendera. Serikali yetu inaelekea kuwa tegemezi mno kwa wale wale waliotutawala, wakiwemo Wajerumani, Waingereza, Wamarekani, Japani na nchi nyingine za “Kundi la nchi nane”. Hivyo serikali yetu inajikuta haina uhuru wa kuamua mambo yake yenyewe, kwa mfano uwezo wetu wa kufanya maamuzi kuhusu mambo ya msingi ya jinsi ya kugawa rasilimali zetu ni mdogo na umefifishwa na hali yetu ya utegemezi.

Mfano mwingine unahusu mapambano yetu kuhusu umilikaji wa ardhi, jambo ambalo ni kati ya yale yaliyowasukuma Watanganyika kusimama kupigania uhuru wao. Muda mfupi baada ya uhuru, Serikali ilipitisha sera ya ardhi ambayo ilitambua umiliki wa ardhi kuwa wa jamii na kuwazuia wageni wasimiliki ardhi. Sera hii ya ardhi imekuwa ikipigwa vita na wawekezaji na watanzania wenye uroho tangu miaka ya 1980, na hatua kwa hatua, Serikali imekuwa ikiruhusu matumizi ya ardhi kwa wageni katika sekta  za kilimo, utalii, uchimbaji wa madini na mabenki yanayowekeza hapa nchi. Hivyo basi, suala la ardhi limeanza kuibuka upya na wanaharakati pamoja na jamii katika sehemu mbali mbali wameanza kujipanga upya ili kulipinga.

Utafiti uliofanywa na Susan Geiger, juu ya Wanawake wa TANU, unaonyesha wazi kabisa kwamba wakati wa kupigania uhuru, wanawake walipambana bega kwa bega na wanaume. Kitabu hiki kilichotafsiriwa na TGNP katika lugha ya Kiswahili kinafichua ukweli kwamba wakati wa kupigania Uhuru, wanawake walikuwa mstari wa mbele; walitembea nchi nzima wakihamasisha watu kujiunga na TANU, walichangisha fedha za kuendesha chama na harakati nyingine za kupigania uhuru, walifanya kazi mbali mbali za kupata kipato ili waweze kupata fedha za kuendesha chama. Hivyo tunapoangalia utetezi wa jinsia na ukombozi wa Mwanamke kimapinduzi ni lazima tuangalie mbele zaidi  ya kabla ya Beijing.

Kitabu cha Susan Geiger, kinatupatia majina mengi ya wanawake waliopigania uhuru. Majina haya hayasikiki tena. Yamezikwa na kufunikwa na mfumo dume. Ingawa jina la Bibi Titi Mohamed linasikika kwa mbali, majina  ya wanawake wengine alioshirikiana nao Dar-es-Salaam, hayasikiki kabisa. Hata mikoani kulikuwa na wanawake walioshiriki harakati za ukombozi wa taifa letu. Kule
Kilimanjaro kulikuwa na Halima Selengia Kinabo, Mwamvita Salim, Zainab Hatibu, Morio Kinabo, Violet Njiro, Elizabeth Gupta, Kanasia Tade Mtenga,Natujwa Daniel Mashamba na Lucy Lameck. Hata kule Mwanza kulikuwa na wanaharakati wanawake waliopigania uhuru wa taifa letu, lakini historia haiwakumbuki  tena. Wanawake hao ni: Agnes Sahani, Aziza Lucas, Tunu Nyembo, Halima Ntungi, Mwajuma Msafiri, Pili Juma, Mwamvua Kibonge, Zuhura Mussa  na  Chausiku Mzee.

Ni wazi wako wanawake wengine wengi walioshiriki harakati za kuleta uhuru wa taifa letu, ni kazi ya Mashirika yanayotetea usawa jinsia na ukombozi wa Mwanamke kuendelea kufanya tafiti na kuibua majina mengine ili kuweka kumbukumbu sahihi ya historia ya taifa yetu.

Kama tutakavyoona wakati wa kutafakari juu ya mchango wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayojishughulisha na masuala ya jinsia na ukombozi wa mwanamke kimapinduzi ni changamoto ya utegemezi. Mashirika mengi au tuseme yote yanategemea fedha kutoka nje ya nchi. Utafiti juu ya Wanawake wa TANU, unatufichulia “siri” kwamba wakati wa kupigania uhuru na miaka michache baada ya uhuru Wanawake wa TANU, walikuwa na uwezo wa kuendesha mambo yao bila msaada wowote kutoka nje au kutoka kwa serikali ya mkoloni. Msimamo huu wa kujitegemea uliwawezesha wanawake kuunda vyama vyao vyenye nguvu kiasi cha kuwatishia “Usalama” wanaume. Uamuzi wa serikali wa kuvivunja vyama hivi vya wanawake mara baada ya uhuru na kutengeneza chama kimoja cha UWT, ambacho kilikuwa chini ya serikali na kupata ruzuku kutoka serikalini ni ishara tosha kwamba vyama hivi vilikuwa na nguvu za kutisha.

Kwenye kitabu cha Susan Geiger, Bibi Titi Mohamed, ananukuliwa akielezea yaliyotokea “ Tarehe 2 Novemba, mwaka 1962, Mheshimiwa Nyerere aliagiza kwamba vyama vyote vya wanawake Tanganyika vivunjwe; yaani, YWCA, Baraza la Wanawake Tanganyika na UMCA, ili viungane kuunda Umoja wa Wanawake wa Tanganyika (UWT)”

Kwa maoni ya Bibi Titi Mohamed, kuvunjwa kwa vyama vya wanawake na kuanzisha chama kimoja cha UWT kilichokuwa chini ya  CHAMA na Serikali kulidhoofisha maendeleo ya kasi ya ukombozi wa wanawake na usawa wa kijinsia katika taifa letu huru. Utegemezi uliminya uhuru wa wanawake kutoa maoni na kufanya mambo yao kwa uhuru. Wanawake wengi wa TANU, hawakuwa na elimu ya juu, waliongozwa na hekima, busara, kuona mbali lakini hasa na uzalendo. Pamoja  na kutokuwa na elimu ya juu wanawake wa TANU waliona wazi tishio la kuwa  tegemezi; walilipinga wazo hilo kwa nguvu zote, lakini walizidiwa nguvu na vijana wasomi. Usomi wao haukuwasaidia kuona tishio kubwa la utegemezi. Kama anavyoelezea Bibi Titi “UWT ilitaka wizara ilipie semina na walimu waliokuwa wakitoa mafunzo kwa wanawake”. Ukaanza ugonjwa wa posho na kutegemea misaada hadi leo hii.

Bibi Titi anaendelea kuelezea makosa yaliyopelekea kudhoofisha nguvu za wanawake wa TANU; “ Wanawake wengi, vijana na wasomi waliokuwa kitovu cha uongozi UWT, waliteuliwa kutoka taasisi na wizara za serikali, kutafuta fedha, kutoa miongozo katika mafunzo na warsha za uongozi, na katika miradi ya lishe…”

Hivyo kwa njia hii ule uwezo wa wanawake wa kujitafutia fedha za kuendesha mambo yao wenyewe ikawekewa kizingiti.

Susan Geiger, katika kitabu chake anasema hivi kuhusu hali hiyo:
Sasa ni dhahiri kwamba UWT haikuwa mwendelezo wa harakati za wawawake wa TANU. Mkutano Mkuu wa Wanawake wa Afrika uliofanyika Dar-es-Salaam mwaka 1962, uliweka wazi katika rasimu ya katiba yao kwamba UWT ni ya kupigania ukombozi wa wanawake ili waweze kushiriki katika shughuli za -kijamii na za kisiasa Afrika. Lakini Nyerere na washauri wake waliamua kwamba wanawake walihitaji kuendelea na kuendelezwa, na kwamba vikundi vilivyokuwa tayari vinafanya kazi hii viungane chini ya chama kimoja kitakachoshirikisha wawawake wote na kudhibitiwa na serikali. Msomi mmoja alipatwa na mshangao kuwa mara baada ya uhuru, wanawake wamekuwa wajinga na walio nyuma kimaendeleo. Suala la namna ya kuhamasisha wanawake likawa tatizo mara baada ya uhuru. Hiyo ilikuwa kejeli”.
                  
La kustaajabisha zaidi ni mfumo dume uliodumaa wakati wa kupigania uhuru na kuibuka tu mara baada ya Uhuru. Katika kitabu cha Susan Geiger,  Bibi Titi, ananukuliwa akieleza mawazo ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii wakati ule juu ya wanawake: “ Akizungumza kwenye mkutano siku ya  pili, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Bwana Mgonja, alizungumza katika njia iliyofifisha ari ya siasa kwa wanawake na kuimarisha mamlaka ya serikali. Wakati kitengo cha Wanawake kilikuwa kinahamasisha wanawake wajiunge katika harakati za kujenga taifa, Mgonja aliwaambia wanawake kwamba wakilea watoto watakuwa wamelea taifa zima. Aliwasifu wanawake wa juhudi zao katika kupigania uhuru, lakini kwa sasa walichotakiwa kufanya ni kulima, kufuga kuku, kuchimba visima na kupanda miti pamoja na  kushiriki katika kisomo cha watu wazima. Mgonja alionya kwamba itabidi utamaduni wa Kiafrika ukuzwe, kwani wakoloni waliudharau”.

Mgonja, alikuwa akiufufua Mfumo Dume, uliokuwa umedumaa wakati wa kupigania uhuru. Kwa maoni yake kuukuza utamaduni wa Mwafrika ni kuendeleza mfumo dume. Inaelekea hapa ndipo tulipoteleza katika suala zima la usawa wa kijinsia. Anavyosimulia Bibi Titi Mohamed, katika kitabu cha Susan Geiger, ni kwamba idadi kubwa ya wanaume waliunga mkono msimamo wa Mgonja, wa wanawake kurudi jikoni baada ya kupigania uhuru. La kushangaza zaidi ni kwamba hata wanawake vijana wasomi waliunga mkono mawazo ya Mgonja, maana wanawake wa TANU waliopigania Uhuru walikuwa tishio.

Bibi Titi Mohamed anaelezea: “ Kati ya viongozi wanaume, aliyeunga mkono wazo la usawa kwa wanawake alikuwa Nyerere. Yeye alikuwa ameshuhudia wanawake. Hata tuliposema huko bungeni kwamba wanaume waadhibiwe kwa kuwapa wasichana mimba, Nyerere alisimama kidete nyuma yetu…. Kati  ya wanawake wachache bungeni (tuliopigania suala hili) tulikuwa mimi, Lucy, Barbara Johansson na mwanamke mwingine aliyekuwa ameolewa na Mgoa huko Amboni, Tanga. Wanaume walitukasirikia, Nyerere alisema ni lazima sheria hiyo ipite, ili wanaume wanaolaghai wasichana na kuwapa mimba walipe faini, wafungwe au watunze hao watoto”

Hivyo wakati wa kutafakari miaka hamsini ya Uhuru wetu, ni lazima tuchunguze kwa makini yale yaliyopelekea kufuta na kufunika historia ya ukombozi iliyoongozwa na wanawake. Kwa nini mfumo dume ulidumaa wakati wa kupigania uhuru na kuibuka mara tu baada ya Uhuru? Harakati za wanawake wa TANU zilisambaa hadi vijijini, je haraka za siku hizi zinakwenda hadi vijijini?

Kama tutakavyoona kwenye tafakuri yetu ni kwamba kati ya changamoto kubwa ya Mashirika mengi yasiyokuwa ya kiserikali ni kujikita mijini na kusahau kabisa kutandaa hadi vijijini. Wakati inaanzishwa UWT, Oscar Kambona alionya umoja huo kutandaa hadi vijijini. Bibi  Titi, anaeleza katika kitabu cha Susan Geiger:

Oscar Kambona, aliyekuwa Waziri wa Tawala za Mikoa, ndiye pekee aliyezungumza kumuhimu wa Kitengo cha wanawake, ….Alisema kuwa wanawake wanahitaji kufanya kazi kwa bidii, kwani hakuna  taifa linalodhaniwa kuendelea kama wanawake hawajaendelea. Kambona alisisitiza kwamba maendeleo ni lazima yawe ya vijijini na mijini. Viongozi wa UWT walishauriwa kurudi vijijini kuweka mipango ya shughuli na siyo kukazania sehemu za mijini tu”

Ushauri wa Oscar Kambona, haukufuatwa na UWT na hadi leo hii mashirika mengi yanayotetea usawa wa Jinsia na ukombozi wa Mwanamke kimapinduzi yamejikita mijini. Ingawa si kawaida kuanza tafakuri na hitimisho, ni vyema kuzingatia ushauri wa Oscar Kambona, wakati tunajiandaa kuanza safari nyingine ya miaka hamsini ya Uhuru wetu.

Na,
Padri Privatus Karugendo.
+255 754 633122