MAKALA HII ILICHAPISHWA KWENYE GAZETI LA RAI 2005
FISADI NA MWENYE VIRUSI NANI ZAIDI?
Watanzania wanaotaka kuwania urais wa taifa letukupitia chama tawala cha CCM, wameendelea kujitokeza.Ingawa ni haki ya kila Mtanzania kuwania kiti chaurais, tunaelekea kuifanya nafasi hii kama kitu chamzaha! Washabaki wameanza kutabiri ni nani ataibukamshindi. Kila mtu anajitahidi kutoa sababu zake. Jambolinalosikitisha yale yote yanayojadiliwa kuhusuwagombea, hakuna linalogusia mambo ya msingi.Majadiliano yanabaki katika ngazi ya kuangalia sura yamtu, mavazi yake, kabila lake, urefu wake, unene wake,uwezo wake wa kuongea Kiingereza, ukasuku wake nauhodari wake wa kuwashawishi wanunuzi wa taifa letu!Hatuiingii ndani zaidi kuchunguza, sura nzuri ina ninindani yake. Mavazi yanayovutia na yenye bei kubwayamefunika nini? Urefu wa mtu unamaanisha urefu waakili yake na ufupi wa mtu unawakilisha ufupi wa akiliyake? Uwezo wa kuongea Kiingereza unasaidia kuletamaendeleo au unasaidia kuliuuza taifa letu? Ni kipikinamfanya mtu awe wa maana na mwenye thamani kubwakatika taifa? Ni mavazi, Kiingereza, kabila, maumbileya mwili au fikra pevu iliyonolewa kwa njiambalimbali, je ni uzalendo, uwajibikaji, upeo wa kuonambali, kipaji cha kuchambua mema na mabaya kwa manufaaya taifa? Kuitawala na kuiongoza nchi si jambo la mchezo. Nakuitawala nchi si jambo ambalo kila mtu anaweza. Huuni ukweli ambao ingawa ni mchungu ni lazima tuukubali.Waingereza wana neno linaloitwa " conspicuous". Maanayake ni kuonekana wazi wazi, uzuri unaochomoza nakuonekana wazi miongoni mwa mambo mengi mazuri. Kituau mtu aliye " Conspicuous" hana utata. Ndege mweusiakiwa miongoni mwa ndege weupe, anaonekana haraka nawala hakuna utata wa kumtambua. Na wala mtu hawezikuanza kujadili, labda kama mtu ana ugonjwa wakutotambua rangi mbali mbali. Vilevile ndege mweupeakiwa miongoni mwa ndege weusi hana utata wowote.Anaonekana haraka. Hata ukiwa mbali utamuona. Rais, nilazima awe " Conspicuous". Ni lazima achomoze miongoni mwa wengi. Hili si jambo la utata. Inawezekanawakawepo watu wawili au watatu ambao ni "Conspicuous"kwa upande wa utawala na uongozi. Lakini vigezovikiwekwa wazi ni lazima mmoja achomoze zaidi yamwingine. Hili halina haja ya kutumia pesa, manenomengi na mbinu chafu za kupakana matope. Mtu"Conspicuous" wa kuliongoza taifa, atachomoza wazihata kwa kipofu!Mtu mwenye vision, msafi, asiyekula rushwa, mbunifu,mwenye kipaji cha uongozi, msomi na mwelevu, mwenyehekima, busara na mzalendo ni lazima achomoze zaidi yakasuku. Tujuavyo, kasuku hana ubunifu wowote, kaziyake ni kurudia aliyoyasikia bila kubadilisha walakuongeza kitu chochote. Mashairi ya Kipanga, yamheshimiwa Khatib, yanaelezea vizuri tabia ya kasuku.Kasuku wa kweli kweli anaweza kuwa na faidia nahasara. Faida, kama yule aliyemtangulia alikuwa nikiongozi aliyetukuka kwa kulitanguliza taifa mbelekabla ya kitu kingine. Hasara, kama kiongozialiyemtangulia alikuwa hasara tupu. Kasuku wa bandiani wa hatari zaidi, maana siku atakapoyaachia makuchaaliyokuwa ameyaficha, ni kilio na kusaga meno. Silengo la makala hii kuelezea tabia za Kasuku. Mwenyemacho haambiwi tazama na mwenye masikio hakumbushwikusikiliza. Kuendeleza juhudi za Rais Mkapa, sidhambi. Swali ni je, Mkapa ni Alfa na Omega? Walewanaotaka kutawala taifa letu kwa kuendeleza kazialiyoianzisha Rais Mkapa, ni maroboti? Hawanachochote vichwani mwao? Mwenyezi Mungu, kawaumba kwamakosa? Kasuku kwa ukasuku wake hawezi kuwa"Conspicuous". Kasuku hawezi kuitawala nchi! Hii hainamaana kwamba hawezi kuiingia madarakani, anawezakuiingia kwa mizengwe, kwa nguvu za dola na kwakutumia mapesa. Dhambi hii itamtafuna yeye na vizazivyake. Kiongozi wa namna hii si "Conspicuous", hasarazake zinajulikana dunia nzima na sina haja ya kutoamifano!Mbali na Ujana, Uzee, Ukabila, Dini, Kisomo, sifaambazo watanzania wamejiwekea kuwapima wagombea niafya njema. Hii ni sifa nzuri ingawa haitoshi kumfanyamtu kuwa "Conspicuous". Wengine wameenda zaidi kusemakwamba wale wote wanaotaka kuwania urais wa taifa letuni lazima wapime afya zao. Ingeishia hapo,ingeeleweka bila utata na bila magomvi. Kila Mtanzaniaana wajibu wa kupima afya yake. Si kusubiri wakati wauchaguzi. Kinachokera ni kwamba mtu atakayegundulikakuwa na virusi vya UKIMWI, hafai kuwa rais?Hoja hii inatoka wapi na sababu zake ni nini? Labdawatu wana wasiwasi kwamba rais mwenye virusi atakufaharaka na kulishabishia taifa hasara ya kurudiauchaguzi mkuu kwa kipindi kifupi? Labda kwamba raismwenye virusi ataleta aibu kwa taifa? Kama hili lamwisho ni kweli, basi juhudi zote zinazofanywa naTaifa juu ya UKIMWI, ni kazi bure! Tunasema wenyevirusi wasibaguliwe, kuna kampeni na ushauri nasahakwamba tukomeshe unyanyapaa. Kumzuia mtu asigombeeurais, ubunge au udiwani kwa vile ana virusi vyaUKIMWI, si ubaguzi na unyanyapaa?Hapa kuna ugomvi mkubwa, ni lazima matamshi kama hayana fikra hizi potovu tuzishikie bango. Yafanyikemaandamano nchi nzima kulaani fikra hii potovu. Walewote walio kwenye mstari wa mbele katika harakati zakupambana na UKIMWI, ni lazima kushikamana ilikuishinikiza serikali au kikundi chochote chawendawazimu wenye fikra hii potofu kuiacha mara moja!Kwanini kiongozi mwenye virusi vya UKIMWI, aonekanekuleta aibu kwenye taifa letu? Mbona watu hawaoni aibukuliuza taifa letu, hawaoni aibu kufanya mikatabahewa? Mbona hawatambui kwamba hao wanaonunua taifaletu wanatucheka. Hii aibu mbona hatuioni. Mbonahatuoni aibu kuwa na vijana wadogo Wazungu wasiokuwana uzoefu wowote wamejazana kwenye kila wizara eti ni" technical advicers". Kazi wanazozifanya ziko kwenyeuwezo wa watanzania wengi wanaokoswa ajira. Hii si niaibu kubwa kuzidi ya mwenye virusi vya UKIMWI?Wagombea, wapime afya zao kama ilivyo wajibu wa kilaMtanzania. Atakayegundulika ana virusi vya UKIMWI,ajitangaze. Hii imsaidie yeye mwenyewe kujishughulikiana kujijali, na isaidie jamii nzima kwa upande wakuzuia maambukizo. Heshima yake na shughuli zakulijenga taifa ziendelee kama kawaida. Kwa namna nyingine Rais, mwenye virusi anawezakupambana vilivyo na ugonjwa huu wa hatari. Atakuwaanaguswa kwa namna ya pekee maana na yeye atakuwamwaathirika. Hadi sasa viongozi wetu wanafanya mchezo tu bila kuangalia kwa mbali ni tishio gani la ugonjwahuu liko mbele yetu. Wanaendeleza urafiki na kujikombakwa viongozi wa dini, na sasa hivi kwa vile niuchaguzi, hata wenye misimamo ya kuunga mkono matumiziya Kondomu, kama Mheshimiwa Sumaye, watakwenda kinyumena nafsi zao ili watafute kuungwa mkono na viongozi wadini.Kuwa na virusi vya UKIMWI, si kufa. Mtu anaweza kuwana virusi vya UKIMWI, akaendelea kuishi zaidi ya miakakumi. Na wala kuwa na virusi vya UKIMWI haina maana yamtu kutokuwa na thamani tena katika jamii.Tumeshuhudia watu mbali mbali katika nchizilizoendelea wakiishi na virusi vya UKIMWI nakuendelea kushikilia madaraka makubwa katika serikalizao.Si lengo la makala hii kumtetea mtu yeyote. Wagombeawote wameambiwa wapime. Hakuna mwenye uhakika ni ninikitajitokeza, hakuna wa kujiamini hadi baada yakupimwa. Na Waswahili wanasema, umdhaniaye ndiye siye!Ni ukweli kwamba kuna wagombea wanaonyoshewa kidolekwamba wana virusi vya UKIMWI. Na ni ukweli kwambaimeandikwa kwenye vyombo vya habari kwamba wagombeawapime afya zao. Ni ukweli pia kwamba wenginewameogopa na kukimbilia hospitali kujipima. Si lengola makala hii kuwatetea. Hoja ni kwamba hata mgombeaakigunduliwa ana virusi, ana haki ya kuchaguliwa kamayeye anafaa. Kama ana vision, kama ni mzalendo, kamasi fisadi, kama hakushiriki kwa namna yoyote ilekuliuza taifa letu, kama anaweza kuutoa uhai wake kwaajili ya maendeleo ya taifa letu. Hata akitawala mwakammoja akafa, hatuwezi kuwa tumepata hasara. La msingisi mtu amekaa miaka mingapi madarakani, ni amefanyanini wakati akiwa madarakani. Mtu anaweza kukaa miakamingi madarakani, lakini akawa amezalisha hasara tupukwa taifa. Tunawakumbuka akina Mobutu,Bokassa hata naIddi Amin, walifanya nini cha maana kwa kipindikirefu madarakani.Keneddy, aliitawala Amerika, kwa kipindi kifupi, hadileo jina lake linavuma na mchango wake unaheshimikadunia nzima. Pia imekuja kugundulika kwamba huyualikuwa mtu mwenye ugonjwa uliokuwa unamsababishiamaumivu makubwa kiasi kwamba ingegundulikaasingeendelea kutawala. Lakini yeye kwa vile alikuwana uzalendo wa kulitumikia taifa lake alivumilia nakuyaficha maumivu yake hadi pale risasi ilipoyasitishamaisha yake. Vinginevyo angeendelea kutawala akiwaanaishi na ugonjwa.Yesu Kristu, alifanya utumishi wake kwa kipindi chamiaka mitatu tu. Ni kipindi kifupi. Lakini kwa kipindihicho aliweza kufanya yanayokumbukwa hadi leo hiibaada ya miaka elfu mbili ya kifo chake!La msingi si unafanya kitu kwa muda gani, ni unafanyakwa lengo gani na kwa moyo upi. Kama unalengakuwatumikia watu na kuwaletea maendeleo kwa moyo wakujitoa, usiokuwa na ubinafsi, visasi, na ufisadi nilazima unachokifanya kistawi kama mti uliowekewambolea na kumwagiliwa maji, ni lazima ustawi kama mtiwa mchungwa, mkahawa, wenye afya nzuri na wenyematunda mengi na matamu. Hata kama kazi hiyo utaifanyakwa dakika tano.Kama ni uamuzi wa taifa letu kwamba wagombea wenyevirusi hawafai kuliongoza taifa. Tutakuwa tumekoseakama taifa. Ni lazima tuwaangukie wenye virusi nakuwaomba msamaha. Tuwaombe radhi watoto yatimawaliopoteza wazazi wao kwa ugonjwa huu wa hatari.Tuwaombe radhi wafadhili wanaotoka mapesa ya kuendeshasemina, makongamano na mikutano ya kuelimisha kuhusuUKIMWI, kuhusu kutowabagua wenye virusi na kuhusuunyanyapaa. Pesa zao tumezitumia bure, tumeshindwakupiga hatua, bado tunawabagua wenye virusiTaifa kama Tanzania, ambalo hata kwenye miji mikubwabado watu hawana huduma ya maji. Jijini Dar-es-Salaam,watu wanamaliza miezi mitatu hadi minne bila kupatahuduma ya maji. Watu hawana huduma ya umeme. JijiniDar-es-Salaam, Mwanza na miji mingine mikubwa kamaArusha, umeme unakatika ovyo bila taarifa, kazi zawatu zinasimama, vyombo vya watu vinaharibika. Magarimengi yaliyo kwenye miji yanatishia maisha ya watuhasa kwenye makutano ya barabara kuu. Serikaliinayowajali watu wake, ingeweza kujenga barabara zakupita juu au chini kwa ajili ya waendao kwa miguu.Taifa ambalo pamoja na utajiri wote halijafanikiwakuwalisha watu wake, kuwasomesha watu wake, kuwapatiahuduma za matibabu watu wake. Taifa ambalo linajua nakutambua kwamba yote hayo yanatokea kwa sababu yaufisadi, rushwa, uzandiki, uchu wa madaraka, ubinafsi,ulemavu wa fikra, bado linashawishika kumtanguliza mtufisadi kuitawala nchi na kuchimba mizengwe ya virusivya UKIMWI! Ni mchawi gani ameliloga taifa letu laTanzania?Adui yetu si virusi vya UKIMWI, bali ni mduduasiyeonekana. Mdudu anayeshambulia maadili yetu. Mduduanayesababisha upofu, tukaacha kuona ukweli. Mduduanayechochea uzinzi usiobagua watoto, wakubwa,wanaume, wanawake, viongozi wa serikali, viongozi wadini. Mdudu huyu asiyeonekana anayechochea rushwa nakutowajibika na uvivu. Mdudu huyu anayeshambulia fikrazetu na kuzisababishia ulemavu mkubwa wa kujikana sisiwenyewe, tukazikana rangi zetu, majina yetu, lughayetu, mazingira yetu na kuiuza nchi yetu. Mduduanayechochea kasi ya ubaguzi, ukabila na udini. Mduduhuyu ndiye mwenye hatari kuliko hata virusi vyaUKIWMI. Mdudu huyu ameyatafuna mataifa mengi katikabara letu la Afrika, na sasa anatunyemelea sisi kwakasi na bila kificho!Mtu aliye "conspicuous", ambaye kila mtanzaniaanamuona, mwenye uwezo wa kupambana na mduduasiyeonekana, ndiye anayefaa kuliongoza taifa letu.Tukikalia upuuzi, ubaguzi na unyanyapaa wa fulani anavirusi vya UKIMWI, fulani ni mtoka mbali, fulani nikijana, fulani si mzee! Tutaanguka kwenye ajalinyingine ya kumwendeleza mdudu asiyeonekana kwakipindi cha miaka mingine kumi. Hoja yangu inabakipalepale: Fisadi na Mwenye virusi asiyekuwa na doa, ninana zaidi?Na,Padri Privatus Karugendo.
0 comments:
Post a Comment